1000 Jobs (Doctors) at Ministry of Health | AJIRA MPYA ZA MADAKTARI 1000 SEKTA YA AFYA 2020

By | March 25, 2020
AJIRA MPYA SEKTA YA AFYA 2020

MoHCDGEC Application Portal, Ajira Za Afya Application System, Health Sector Jobs 2020, Ajira Wizara Ya Afya 2020

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA MPYA ZA MADAKTARI 1000

The President of the United Republic of Tanzania issued a Notice on assignment of Ministerial responsibilities (Instrument) vide Government Notice No.144 of 22nd April, 2016. In that Instrument, the President has created a Ministry of Health,Community Development, Gender, Elderly and Children which is mandated for formulation of the following below things for the development of Tanzania:-

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA MPYA ZA MADAKTARI 1000

Katika Utekelezaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya) kupitia kibali cha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na.

FA.97/128/01/”A”/51 cha tarehe 16 Machi, 2020; Inatangaza nafasi elfu moja (1,000) za Ajira Mpya za Kada ya Madaktari Daraja la II kwa mchanganuo ufuatao; 

Na. TAASISI IDADI YA NAFASI
1. Ofisi ya Rais,TAMISEMI (Hospitali za Wilaya) 610
2 Wizara ya Afya (Hospitali za Rufaa za Mikoa) 306
3 Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) 40
4 Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) 20
5 Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) 10
6 Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) 7
7 Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) 7
  JUMLA   1,000

Sifa za Mwombaji

 1. Awe raia wa Tanzania
 2. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi Umri wa miaka 45
 3. Awe hajawahi kuajiriwa Serikalini na kupata cheki namba na endapo mwombaji atakuwa alishaajiriwa Serikalini na kupata Cheki Namba,  atatakiwa kuzingatia Utaratibu wa uhamisho au kurejea katika Utumishi wa Umma baada ya kuacha kazi kama ilivyobainishwa kwenye Waraka Na. CCB.228/271/01 wa tarehe  07 Agosti, 2012.

Maombi yote yaambatishwe na nyaraka zifuatazo;-

 1. Nakala ya cheti cha kuzaliwa
 2. Nakala ya cheti cha Kidato cha Nne/Sita
 3. Nakala ya Vyeti vya Taaluma (Cheti na Transcripts) 
 4. Nakala ya cheti cha Usajili Kamili (Full Registration) 
 5. Waombaji waliosoma nje ya Nchi waambatanishe na Ithibati (Accreditation) kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
 6. Cheti cha Mafunzo kwa Vitendo (Internship)
 7. Maelezo Binafsi (CV)
 8. Picha ndogo (passport size) mbili za hivi karibuni

Maelezo ya ziada kuzingatia;

 1. Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa wa madaktari. Hivyo utatakiwa kuchagua maeneo matatu (3) ambayo ungependa kupangiwa endapo utafanikiwa kupata nafasi hiyo; Aidha, hakutakuwa na kubadilisha kituo pindi utakapopata nafasi hiyo
 2. Nakala za Vyeti vyote vithibitishwe na Mahakama au Wakili
 3. Waombaji wanaojitolea katika mikoa mbalimbali waambatishe barua inayomtambulisha kutoka kwa Mganga Mkuu/Mfawidhi wa Mamlaka husika.
 4. Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao (online) kupitia mfumo wa kielektroniki unaopatikana kupitia anuani ifuatayo ajira.moh.go.tz.
 5. Maombi yoyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa moja ofisini hayatafanyiwa kazi.
 6. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 10 Aprili, 2020 saa 9.30 Alasiri.

Tangazo hili linapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto www.moh.go.tz

NAFASI ZA KAZI WIZARA YA AFYA
Dkt. Zainab A.S. Chaula

KATIBU MKUU (AFYA)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *